Waheshimiwa madiwani wilayani malinyi wametakiwa kuwahimiza wananchi kuchangia jenzi wa zahanati kwa kila kijiji ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Kauli hiyo imetolewa na mkrugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Marcelin Ndimbwa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali .
Ndimbwa amesema kuwa wananchi pasipo kuhimizwa ushiriki huwa ni mdogo hvyo ametoa rai hiyo kwao kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa maendeleo.
Hata hivyo amewapongeza idara ya elimu msingi pamoja na kamati kwa ujumla kwa matokeo mazuri ya darasa la saba mwaka huu kwani kimkoa imeshika nafasi ya kwanza kati ya wilaya 9 kwa wastani wa asilimia 82.97.
Wakati akifunga kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri hiyo mh Fadhili Liguguda amewashukuru n kuwapongeza watendaji wote kwa pamoja kwa kuonyesha vitendo kwa kasi zaidi kuliko maneno na kutatua changamoto ili kuleta mafanikio zaidi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.