Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mh. Mathayo Masele amezindua rasmi baraza la wazee la wilaya siku ya Jumatatu tarehe 6 julai 2020 ,baraza hilo limeundwa siku hiyo ya tarehe 6 julai chini ya usimamizi wa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Hawa Lumuli Mpossi ,ambapo limehudhuriwa na wawakilishi kutoka katika kila kata za wilaya ya Malinyi jumla yao wakiwa ni wajumbe 25.
Katika baraza hilo umefanyika pia uchaguzi wa viongozi ambapo ndg. Raphael Mkumbila wa kata ya sofi amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza hilo la wazee,ndg.Augustino Chilumanga kutoka Igawa makamu mwenyekiti . pia Bi.Dafrosa Libonge kutoka Mtimbira katibu,na ndg. Isaya Ng’ulile wa Malinyi kuwa katibu msaidizi. Ndg. Teifrid Njige kutoka Biro amechaguliwa kuwa Mtunza Hazina wa baraza hilo.Mwishowe wawakilishi katika baraza la madiwani kwa nafasi ya wanaume na wanawake imeshikwa na ndg .Ngangaa Fulgence wa Sofi na kwa wanawake ni Bi. Ernesta Mchanga wa Njiwa.
Akizungumza katika baraza hilo Mh. Masele amewafahamisha wazee jitihada mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri pamoja ofisi ya mkuu wa wilaya katika kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya baada ya kupokea shilingi million mia tatu kutoka serikalini.pia amewaeleza jitihada zinazofanywa kukabiliana na uharibifu wa barabara uliotokana na mvua.Mwisho amewahakikishia wazee juu ya uwepo wa dirisha la wazee mara hospitali ya wilaya itakapoanza kutoa huduma.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.