Katibu tawala wilayani Malinyi Lameck Lusesa amefungua uzinduzi wa kusajili watu wenye mahitaji ya namba ya utambulisho wa mlipakodi TIN NAMBA .
Uzinduzi huo umefanyika leo na kuendeshwa na shirika la mapato Tanzania TRA maeneo ya malinyi mjini na kuhudhuliwa na wafanyabiashara mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa katibu tawala aliyemwakilisha mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.
Wakati akizindua usajili huo kwa vitendo Lusesa amewataka viongozi mbalimbali kuhamasisha wafanyabiashara kusajili biashara zao kwa hiari kwani kupata TIN NAMBA hakuna gharama yoyote.
Aidha ameongeza kuwa ni vyema mfanyabiasha anapouza bidhaa kutoa risiti na mtu kudai risiti pale anaponunua bidhaa kwani kwa kufanya hivyo italeta uzalendo kwa wilaya katika ukusanyaji wa mapato.
Hata hivyo kaimu meneja mkoa morogoro Joseph Shirima amesema kuwa lengo kubwa la kufanya usajili huo ni kuleta huduma karibu na wananchi.
Barabara ya Kuelekea Kanisa la Katoliki Kipingo
Postal Address: P.O.BOX 18 Malinyi
Telephone: 255
Mobile: 0755388218
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Hatimiliki©2017 MALINYIDC Haki zote zimehifadhiwa