Kamati ya madiwani ya fedha ,uongozi na mipango wamekagua miradi ya maendeleo katikati ya mwezi januari,miradi iliyotembelewa ni jengo la makao makuu ya Halmashauri linalojengwa eneo la kijiji cha Misegese,wakiongea na meneja wa Mradi huo bwana Abdul Saidi Kambwela amesema kuwa mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa 29 novemba 2018 lakini kutokana na changamoto za mvua za mwaka uliopita waliongezewa muda wa miezi sita na hivyo jengo hilo linategemewa kukabidhiwa tarehe 29 may 2019, Meneja huyo ameeleza kuwa jengo hilo mpaka sasa limefikia asilimia 60%.
Hata hivyo pamoja na ujenzi huo kuendelea kuna changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ikiwemo ubovu wa barabara unaosababishwa na mvua ,hivyo kusababisha vifaa vya ujenzi kushindwa kuja kwa wakati.
Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya cha Tarafa ya Ngoheranga kilichopo katika kijiji cha Ngoheranga,pia wamekagua majengo ya zahanati ya kijiji cha Biro.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.