Kamati ya fedha ,uongozi na mipango ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika eneo la Misegese leo tarehe 29/08/2018 miradi iliyotembelewa ni ,Ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri, ujenzi wa madarasa mawili katika shule Tarajali Saratogo, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo.
Ujenzi wa jengo la makao mkuu ya halmashauri ya wilaya ya Malinyi unajengwa na mkandarasi NHC(National Housing Co-operation) wakiambatana na mhandisi mshauri TBA(Tanzania Building Agency) kwa gharama ya sh billion 3.8 kutoka serikali kuu. Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili katika shule tarajali ya Saratogo eneo la misegese, umegharimu sh milioni ishirini kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri ikijumuisha na nguvu za wananchi, pia vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo vinajengwa kwa fedha kutoka serikali kuu shilingi milioni 66,600,000/= P4R , vilevile madiwani hao walitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Hospital ya Wilaya katika kijiji cha Misegese kitongoji cha Mwembeni.Miradi hiyo ya madarasa katika shule zote mbili imefikia hatua ya mwisho ya kumaliziwa.
Barabara ya Kuelekea Kanisa la Katoliki Kipingo
Postal Address: P.O.BOX 18 Malinyi
Telephone: 255
Mobile: 0755388218
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Hatimiliki©2017 MALINYIDC Haki zote zimehifadhiwa