Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 29.04.2018 katika ukumbi wa halmashauri, Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Malinyi Bw. Henry Chinyuka alitoa mada inayohusu Kansa ya Shingo ya Uzazi. Aliwajuza wajumbe athari za kansa hiyo ikiwa ni pamoja na vifo kwa akina mama wengi hapa nchini. Alitoa uelewa kuwa chanzo kikubwa cha vimelea vya ugonjwa huo ni wanaume ambao hubeba vimelea na kuviacha kwa akina mama (wanawake/wasichana) wakati wa tendo la ndoa. Aliwajuza kuwa wanaume wasitahiriwa hubeba vimelea hivyo kwa wingi ukilinganisha na wale waliotahiriwa, hivyo alisema kuna kampeni "Vua Suweta" inayohamasisha wanaume kutahiriwa inaendeshwa na serikali na itakuja hadi Malinyi. Wakati wa kuhairisha kikao hicho Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi Bw. Lameck Lusesa aliwaomba wajumbe wa kikao hicho kwenda kutoa elimu waliyopata kwenye maeneo wanayotoka ili kujenga uelewa kwa wananchi walio wengi. Pia aliwaomba kushiriki katika Uzinduzi wa kutoa chanjo ya Kansa ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14. Uzinduzi huo utafanyika hapa Malinyi siku ya Jumatatu tarehe 30.04.2018.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.