Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya malinyi ndugu Mussa E. Mnyeti amewataka watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuzidi kuleta maendeleo katika halmashauri.
Mnyeti ameyazungumza hayo leo wakati akizungumza na watumishi wote wa halmashauri ya malinyi pamoja na kufahamiana kwa ujumla na kutoa maagizo aliyopewa na Mh Rais.
Aidha amesema kuwa wakati anateuliwa ameagizwa kuwa miongoni mwa mambo anayopaswa kuyafanya ni pamoja na kusimamia rasilimali watu katika halmashauri kwa kushirikiana na idara husika, ongezeko la mapato pamoja na masuala ya ardhi ili kusiwepo na migogoro.
Kikao hiki ni kikao cha kwanza ikiwa baada ya kuteuliwa na Mh Rais 13 agust mwaka huu na kufanya mabadiliko mbalimbali.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.