Meneja wa Takukuru na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro wametakiwa kuhakikisha kuwa waliogawa na kufanya ubadhilifu wa fedha ndani ya viwanja vya nanenane morogoro wanakamatwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto mh Hamisi Kigwangalla ambaye amemwakilisha makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia suluhu Hasan aliyepaswa kuwa mgeni rasmi kwenye maonesho ya 25 ya sikukuu za wakulima mkoani morogoro.
Kigwangalla amesema kuwa viongozi wote wa shirika la chama cha kilimo Tanzania TASO ambao wamehusika kugawa viwanja na kufanya ubadhilifu wa fedha kwa muda wa miaka 3 wakati wanasimamia shughuli za maadhimisho ya sikukuu za wakulima wakamatwe wawekwe ndani na uchunguzi uendelee ili kubaini kiwango cha ubadhilifu walioufanya.
Aidha ameongeza kuwa kufutiwa usajili pekee kwa shirika hilo haitoshi hivyo ni lazima watoe adhabu ili iwe mfano kwa wengine ili wasiweze kurudia makosa kwani mashirika yamekuwa yakijisahau na kudhani mali ni za kwao pale wanaposhindwa kufanya kazi bali mali hizo huwa ni mali za umma.
Hata hivyo ametoa rai kwa vijana kuwa wajitume na wafanye kazi za kilimo ili waweze kujiajiri kwani kilimo kinalipa na si kusubiri kuajiliwa huku akiongeza siku 2 za maadhimisho ya 8-8 kumalizika tarehe 10 kwani watu bado ni wengi na bidhaa smbzo zimebaki kwa wakulima ambazo zinazoweza kuharika zinunulike.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.