Wahitimu wa darasa la saba wametakiwa kujilinda na kujitunza ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea.
kauli hiyo imetolewa hii leo na mgeni rasmi katika sherehe za mahafari hayo ambaye pia ni afisa uchaguzi wilaya ndugu Christopher Tengeneza katika viwanja vya shule ya msingi nawigo wilayani malinyi.
Tengeneza amesema kuwa wahitimu hao wanapaswa watambue kuwa bado ni wanafunzi hivyo hata warudipo majumbani wafanye yale yote yaliyo ya kimasomo zaidi na wasije kujisahau na kuongeza kuwa wakazidi kujiendeleza kimasomo kwa kusoma masomo ya ziada kwa ajili ya maandalizi ya kuingia kidato cha kwanza mara tuu baada ya kutoka matokeo.
kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Rashidi Kiding'a amesema kuwa waliwapokea wanfunzi hao wakiwa wadogo wasiojua kusoma wala kuandika na hatimaye sasa wanajitambua na wanaojua kusoma hivyo amewataka wazazi wawaendeleze zaidi watoto hao na si kuwatumikisha katika mambo si ya msingi mfano wasichana wa kazi za ndani.
hata hivyo wahitimu hao walianza darasa la kwanza mwaka 2011 wakiwa wanafunzi 153 huku wavulana wakiwa 64 na wasichana 89 na waliobahatika kufanya mtihani wa darasa la saba wakiwa jumla 136 waavulana 58 na wasichana 78 huku waliosalia walikaririr madarasa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.