Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven Kebwe amewataka wakazi wa malinyi kupanda miti ili kuondokana na uharibifu wa mazingira unaojitokeza.
Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha misegese ambao umejumuisha viongozi mbalimbali wa serikali asasi za kidini pamoja na wananchi.
Dr kebwe ameeleza kuwa licha ya uharibifu unaojitokeza kipindi cha mvua lakini pia kumekuwa na uharibifu ambao unasababishwa na wakazi wenyewe hususani kufanya shughuli za kibinaadamu katika vyanzo vya maji.
Hata hivyo amewataka viongozi wa serikali kushirikiana na wananchi kuweza kufanikisha zoezi hilo kwani kingo za miti zinazidi kuharibiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.