Maadhimisho hayo yalianza kwa wafanyakazi kuwatembelea wagonjwa ktika Hospitali Teule ya Lugala. Baadaye wafanyakazi walijumuika kwenye maandamo kuanzia Hospitali ya Lugala hadi Sm. Nawigo ambapo mgeni rasmi alipokea maandamano hayo. Akihutubia katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Malinyi Bw. Marceline Ndimbwa aliwapongeza kwa dhati wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi katika sekta zote kwa kuiletea sifa halmashauri katika nyanja mbalimbali. Alitoa mfano, Malinyi imekuwa ya kwanza kimkoa katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2017/2018, pia wilaya ya Malinyi imekuwa ya kwanza kati ya Halmashauri tisa za mkoa wa Morogoro katika matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi n.k. Hata hivyo katika hotuba yake ametangaza kuwafutia mashtaka ya kiutumishi watumishi wote walikuwa na kesi kwenye ngazi mbalimbali wilayani humo na aliwaomba kurudi katika kazi ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kuinua uchumi wa Wanamalinyi na nchi wa ujumla. Aidha aliwapongeza wafanyakazi kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho hayo na alitoa mapendekezo kwa kamati ya maandalizi kuwashirikisha wafanyakazi toka katika kila kata za Halmashauri yetu ili nao washiriki katika maadhimisho ya Mei Mosi. Pamoja na hayo yote Mgeni rasmi huyo alitoa zawadi kwa wafanyakazi hodari toka kila idara za Halmashauri na kutoka katika taasisi zisizo za kiserikali. TUNAWAPONGEZA WAFANYAKAZI WOTE WA HALAMASHAURI YA WILAYA YA MALINYI KWA KUUNGANA NA WAFANYAKAZI WENZAO DUNIANI KOTE KATIKA KUADHIMISHA MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2018. SOLIDARITY FOREVER (MSHIKAMANO DAIMA)
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.