Jumla ya miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 957,020,477.11 imepitiwa na mwenge wa uhuru katika wilaya ya Malinyi kwa mwaka 2021. Katika miradi hiyo wadau mbalimbali wamechangia ikiwemo halmashauri shilingi milioni 37,wananchi shilingi milioni 16,866,000,serikali kuu shilingi milioni 617,854,977.11 na wahisani shilingi milioni 285,299,500. Aidha katika miradi hiyo,miradi mitatu ilionwa na mwenge huku miradi miwili iliwekewa jiwe la msingi na miradi miwili kuzinduliwa na hakuna mradi uliokataliwa na kiongozi wa mbio za mweng. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya njiwa wenye gharama ya shilingi milioni46.766,mradi wa ghala la kuhifadhia na kuchakata nafaka(MIC RICE MILL) wenye gharama ya shilingi milioni 180,ujenzi wa mradi wa maji Sofi Mission wenye gharama ya shilingi milioni 436 na ujenzi wa jengo la utawala-uthibiti ubora wa shule wenye gharama za shilingi milioni 181.81. Miradi mingine ni ujenzi wa wodi ya watoto wachanga Lugala wenye thamani ya shilingi milioni 104.8,kikundi cha kutengeneza sabuni(Kombola-Malinyi)wenye thamani ya shilingi milioni 7.6 na klabu ya wapinga rushwa shule ya msingi Mwembeni
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.