Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ya Malinyi Ndugu Mussa E. Mnyeti amewasimamisha kazi watumishi sita kuanzia tarehe 5/2/2019 kwa upotevu wa jumla ya shilingi (54,627,000) milioni hamsini na nne laki sita na ishirini na saba elfu. Watumishi hao ni bwana Hamisi kitambulilo ambaye anadaiwa shilingi 19,055,500/= na Bwana Fatehe Nyangasa shilingi 10,863,000/=, Juma Mbulu shilingi 1,129,500/= hawa wote walizipata fedha hizo kupitia makusanyo ya Posi.
Na wengine ambao wamesimamishwa kazi ni Audifesto Lyampawe ambaye ni afisa maendeleo ya jamii anayedaiwa shilingi 15,686,000/= ambayo ni marejesho ya vikundi vya wanawake na vijana,pamoja na Tulia KIhoro naye ni afisa maendeleo ya jamii anayedaiwa shilingi 5,758,000/= fedha za marejesho, na wa mwisho ni Leocadia Semindu mtendaji wa kijiji cha Mchangani anayedaiwa shilingi 2,135,000/=. Watuhumiwa hawa wamekabidhiwa mikononi mwa polisi na wapo rumande.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.