Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Dk. Steve Kebwe alitembelea wilaya ya Malinyi tarehe 08.10.2017 katika ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa wa Morogoro kuhamasisha na kuhimiza wananchi kulima zao pamba. Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa aliambatana na Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania na wataalamu mbalimbali wa sekta ya kilimo ambapo elimu juu ya kilimo cha pamba ilitolewa kwa wananchi. Pamoja na elimu iliyokuwa inatolewa mkuu wa mkoa aliwahakikishia soko la pamba wananchi wa wilaya ya Malinyi. Kwa nafasi yake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba na wataalamu wake walionyesha mifano mbalimbali ya namna bora ya upandaji wa mbegu za pamba. Alisisitiza kuwa kwa upandaji huo ekari moja ya pamba huwa na miche zaidi ya 10800 ambayo ikihudumiwa vizuri ekari hiyo yaweza toa zaidi ya kg 1200 za pamba. Mkutano huo ulifanyika katika kijiji cha Kipingo, kata ya Malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.