Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg Steven Kebwe ameitembelea Wilaya ya Malinyi na kukagua shughuri za CHF. Katika Masafara huo Mkuu wa Mkoa alifuatana na Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Morogoro, na Uongozi wa CHF Mkoa.
Mkuu wa Mkoa alitembelea Zahanati ya Malinyi na Kituo cha Afya cha Mtimbira na kuwaasa Wananchi wajiunge na CHF kwani kwa sasa huduma ni nzuri na upatikanaji wa dawa ni 90% kwa Mkoa wa Morogoro.
Pia alisisitiza Wafanyakazi kuwahi kazini, kutojihusisha na siasa muda wa kazi na pia Wananchi kutunza Mazao waliyoyapata kwa kwa mwaka huu Wilaya ya Malinyi imepata Mvua za kutosha na Mazao ni mengi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.