Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Mathayo Masele amesisitiza utoaji wa Lishe Bora kwa watoto wakati wa kikao cha Tathmini ya Mkataba wa utekelezaji wa AFUA ZA LISHE ngazi ya Kata na Vijiji robo ya pili (OCTOBA-DISEMBA 2020) kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi tarehe 26 februari, 2021.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amemwomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mhe. Hawa Lumuli Mpossi katika kikao kijachokuwepo na ripoti ya kutembelea Kata zote, na kujua ukaguzi wautoaji wa Lishe umefanyika kwa kiasi gani, na wameshauri kwa kiwango gani na udumavu umeisha kwa kiasi gani.
Pia Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka wajumbe wa kamati ya Lishe kuwatambua wadau wote wa Lishe ili kuweza kutokomeza udumavu katika Wilaya ya Malinyi.
Aidha, Afisa Lishe (W) Bwana Samwel Mwita Masiaga amewahimiza Watendaji wa Kata na Vijiji katika kuendesha siku za Lishe katika kila Kijiji na kutoa taarifa za utekelezaji wa AFUA za LISHE kila mara wanapoipata kwa Mwezi na kwa robo mwaka.
Wakati wa wajadiliano Mhe. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mhe. Hawa Lumuli Mpossi alimalizia kwa kuwaelekeza watendaji wa kata wote na Vijiji kuhakikisha ifikapo tarehe 05 Machi, 2021 wawe wamefanya mikutano ya vijiji ya Lishe na kuanzisha sheria ndogo ndogo za lishe kwa kila kijiji.
OFISI ZINAPATIKANA ENDEO LA MISEGESE
Postal Address: P.O.BOX 18 Malinyi
Telephone: 0784502410
Mobile: 0755388218
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Hatimiliki©2017 MALINYIDC Haki zote zimehifadhiwa