Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi kijijini Ngombo
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi bwana Abdallah Hamis Kulega amefanya ziara ya siku moja wilayani Malinyi na kutembelea na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ngombo jumatano wiki hii tarehe 12 disemba.
Akiongea na wananchi naibu waziri huyo ameeleza lengo la ziara ni kujibu kwa vitendo barua ya wananchi wa chama cha wafugaji wa kijiji hicho cha ngombo ,barua iliyomuomba waziri wa mifugo na uvuvi kuja kijijini hapo kusaidia kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji ambao wanavamia eneo la kijiji chao kutoka wilaya jirani,pia kuhusu mipaka ya kijiji cha Ngombo.
Waziri amewaagiza wanakijij hao kuwa watulivu wakati tatizo lao linafanyiwa kazi , wakisubiri Tume kutoka Tamisemi kushughulikia suala lao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.