Zaid ya nyavu haramu 5 (makokoro) na vyandarua 8 vinavyotumika katika kuvua samaki zimeteketezwa na moto hii leo.
wakati wa zoezi hilo ambalo limeshirikisha jeshi la polisi wilaya na ofisi ya idara ya mifugo wilaya Afisa uvuvi wilayani malinyi Joseph Ogare amesema kuwa nyavu hizo si halali kwa uvuvi wa samaki kwani hubeba mpaka vifaranga vya samaki (dagaa) na kupelekea kutoongezeka.
aidha ameeleza kuwa nyavu hizo zilikamatwa katika kijiji cha kipingo na ngombo mto furua huku wakibahatika kuwakamata wahusika 2 na wengine kukimbia na kila mmoja wao alilazimika kulipa faini ya shilingi laki tano.
hata hivyo bwana ogare amezidi kutoa onyo kali kwa wavuvi wa samaki wanaotumia uvuvi haramu ikiwemo makokoro, vyandarua, sumu n.k katika kuvua samaki kuwa kwa yeyote atakayebainika faini ni shilingi milion mbili au kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.