Wananchi wa Wilaya ya Malinyi wameshiriki zoezi la upandaji miti leo tarehe 10/4/2018 ikiwa ni maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa ambayo kimkoa yameadhishwa wilayani hapa katika kijiji cha misegese kando ya mto Furua, maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Tanzania ya kijani inawezekana, tupande miti kwa maendeleo ya viwanda” yamehusisha pia wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya siasa, taasisi za dini, asasi zisizo za kiserika, taasisi za kijamii za utunzaji wa mazingira, Katika kuadhimisha siku hii Halmashauri imejikita katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ambapo miti ilipandwa kando kando ya Mto Furua.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Majula Kasika ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amezindua maadhimisho hayo na kusema zoezi hili ni muhimu kwa kuwa linarudisha uoto wa asili pia ameeleza madhara ya mafuriko yanayotokea yamesababishwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katika kingo za mto, pia baadhi ya wananchi ambao wamebainika wakifanya shughuli za kibinadamu katika kingo za mto huo kama kilimo,ufyatuaji wa matofali, ufugaji na makazi. Kutokana na hilo Mheshimiwa mgeni rasmi ameagiza Kamati za Vijiji za Mazingira zifanye kazi kikamilifu kudhibiti hali hiyo na pia wananchi wote wanaofanya shughuli hizo ndani ya mita sitini za mto waondoke mara moja kwa kuwa ni kinyume cha Sheria Namba 20 ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.
Nae mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Ndugu Ernest Robert Mkongo ametoa salamu za Mkoa na kusema kwamba mazingira sharti yatunzwe ili yatutunze na kila mwananchi awe mlinzi wa kwanza wa mazingira katika eneo lake na amesisitiza kwamba Serikali iko kwenye mchakato kuanza kufanya sense ya miti hivyo amehamasisha zoezi liwe endelevu kwa kizazi kijacho.
Kwa upande mwingine Afisa Misitu wa Wilaya Ndugu Macha amesema kwamba aina ya miti inayostahili kupandwa kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kando ya mto ni miche ya mishasha ambayo ni rafiki wa maji na pia inasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Katika kuhitisha zoezi hili Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mheshimiwa Majula Kasika amesisitika zoezi hili liwe endelevu na liende sambamba na kuanzishwa kwa vitalu vya miche ya miti ili mwakani lengo la kupanda miti milioni moja lifikiwe. Pia ametoa wito kwa wananchi kujishughulisha na kilimo cha zao la korosho kwa kuwa lina tija katika Taifa na pia upatikanaji wa soko ni mkubwa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.