Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Mh. Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndg. John Mtolera akihutubia mamia ya akina mama wa Malinyi waliojitokeza kwa wingi kwenye maadhimosho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya Viwanja vya TRC Malinyi Mjini. Pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanawake kujiunga pamoja ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili katika jamii. Pia alivipongeza vikundi vya akina mama waliofika katika maadhimisho kuonyesha bidhaa wanazozitengeneza katika vikundi vyao. Bidhaa zilizotia fora katika maonyesho hayo ni vikapu, sabuni na mbolea.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.