Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mh. Mathayo Masele amepokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi million kumi na nane kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa CORONA,kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la SOLDERMED chini ya msimamizi wa daktari Peter,iliyofanyika jumanne tarehe 21 april katika Hospitali ya Lugala.
Akikabidhi vifaa hivyo Dk.Peter amesema kuwa lengo ni kushirikiana na serikali na wananchi kwa ujumla katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa CORONA.Vifaa vilivyokabidhiwa ni mashine za kupumulia wagonjwa mbili, vitanda vinne, mabenchi matatu, sanitizer za kunawia mikono, ndoo,Barakoa na vifaa vingine.
Mh. Masele amewashukuru shirika la Soldermed kwa kujitoa kwa moyo kutoa msaada huo mkubwa kwa Wilaya ya malinyi . Akiongea na baadhi ya watumishi wa afya , wakuu wa idara pamoja na viongozi wengine wa serikali mkuu huyo amewaagiza watumishi hao kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu ugonjwa huu wa CORONA na pia amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kuwa wanawatambua wageni wote wanaoingia katika maeneo yao ili kujua namna ya kuwasaidia pale itakapotokea tatizo lolote linalohusiana ugonjwa huu wa CORONA.
Aidha mkuu wa wilaya huyo amempongeza Mganga mkuu wa wilaya kwa juhudi kubwa anayoifanya katika kazi na hasa kipindi hiki cha janga hili la CORONA.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.