Zaidi ya visima vya maji virefu 20 vinAendelea kuchimbwa katika halmshauri ya wilaya ya malinyi.
Wakati zoezi hilo likiendelea katika maeneo mbalimbali wilayani humo kaimu mhandisi wa maji Patrick Ndunguru amesema kuwa awamu ya kwanza ni kuchimba visima na awamu ya pili ni ujenzi wa matenki ya maji.
Aidha visima hivyo vyenye urefu wa mita 120 na 110 vinatekelezwa katika vijiji vyamtimbira, usngule, sofi majiji, sofi mission, kiswago, misegese na kilosa mpepo Chini ya kampuni ya VICTORIA BOREHOLES DRILLING LTD.
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo marcelin Ndimbwa amesema kuwa serikali imetoa zaid ya shilling million 538 99000 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ili kuwez kupunguza adha kwa akina mama kutembea umbali mrefu wakitafuta maji.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.