Wilaya ya malinyi imepokea mradi wa (uhimilishaji) kupandikiza majike mbegu za madume kwa njia isiyo ya asili.
Mradi huo ambao ni mara ya kwanza kuingia katika wilaya hii huku ukiwa na lengo la kuboresha ng’ombe wa maziwa kwa wafugaji wadogo na wakubwa ili kuzalisha maziwa kwa wingi zaidi.
Aidha mradi huo umeshirikisha mafugaji mbalimbali wa ng’ombe wa maziwa wilayani humo na kupatiwa maelekezo ya uhimilishaji ikiwa ni pamoja na kumtambua ng’ombe anayehitaji, aina za ng’ombe, fida pamoja na hasara zake.
Hata hivyo mmoja wa wawezeshaji wa mradi huo Anzigary Balaka amesema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi 45000 kwa anayehitaji kwa ajili ya kuchangia upatikanaaji wa huduma kwani mbegu hizo uhifadhi wake unategemea ubaridi mkali (196 0c) na kusambazwa kwenye mirija midogo ya plastic.
Ameongeza kuwa kila mrija mmoja unakuwa na mbegu za kiume million nane(8) hadi kumi (10) pia matarajio makubwa ya uhimilishaji ni kupata ndama jike zaidi kwa asilimia 99 mpaka 100 ingawaje inawezekana pia kupatikana kwa ndama dume.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.