Halmashauri ya wilaya ya malinyi imesaini mkataba na shirika la nyumba la Taifa NHF pamoj na wakala wa majengo Tanzania TBA.
Mkataba huo wa makabidhiano umefanyika mbele ya uongozi wa halmashauri pamoja na mashirika hayo katika viwanja hivyo vilivyopo kijiji cha misegese tarafa ya malinyi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya hii ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa 11 mwaka huu.
Aidha wakati wa makabidhiano hayo kaimu afisa manunuzi wilaya bi Rachel Mkumbwa amesema kuwa taratibu za manunuzi zilifuatwa na tenda zilitangazwa huku walioomba wakiwa ni shirika la nyumba la Taifa pamoja na Suma JKT na waliokuwa na vigezo ni shirika la nyumba la Taifa.
Mwenyekiti wa Halmashauri Fadhili Liguguda ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha akiwa sambamba na mkurugenzi mtendaji na wakuu wa idar pamoja na mashirika hayo ili kuweza kufanikisha ujenzi huo kwa kipindi chote.
Halmashauri ya wilaya ya malinyi inatumia majengo ya walimu TRC kama ofisi za muda kwa ajili kuendeshea shughuli zao wakati wakisubiri kujengwa kwa majengo yao rasmi ambayo yanatarajia kutumika zaidi ya bilioni 3 kwa awamu ya kwanza.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.