Ilikuwa ni siku ya kukumbukwa sana kwa wana bonde la mto Kilombero yaani wakazi wa wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga pale Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dt. John Joseph Pombe Magufuli alipozindua rasmi daraja liliopewa jina la Magufuli katika mto Kilombero lenye urefu wa meta 384 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 9.1. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 05.05.2018 kwenye Daraja lenyewe la Mafgufuli ila baadaye Mh. Rais alipata nafasi ya kuhutubia wananchi katika uwanja wa viwanja sitini maarufu sana kwa jina la uwanja wa Taifa uliopo mjini Ifakara. Katika hotuba yake Mh. Rais aliwasisistiza wananchi utunzaji wa miundombinu ya daraja hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu. Aidha aliwaeleza kuwa hiyo ni fursa kwao kwa ajili ya kusafirisha mazao/bidhaa kwa ajili ya biashara zinazotoka na kuingia katika wilaya zinazonufaika na uwepo wa daraja hilo. Pia katika hotuba yake aliwapongeza viongozi (Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo) na wanachi wa namna wavyotekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 kwani amejionea miradi mingi katika mkoa wa Morogoro. Pamoja na uzinduzi huo, Mh. Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye urefu wa kilometa 66.9 itakayojengwa kwa kiwango cha rami. Katika uzinduzi huo Mh. Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano ndg. Makame Mbalawa aliwaeleza wanachi wa wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutafuatiwa na ujenzi wa barabara ya Ifakara - Lupiro - Malinyi - Lumecha itakayounganisha wilaya hizo na mkoa wa Ruvuma.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.