Watendaji wote katika halmashauri wametakiwa kutoa ushirikiano kwa maafisa habari juu ya uwekaji wa taarifa katika tovuti za halmashauri zilizofunguliwa.
Hayo yameelezwa na mgeni rasmi ambaye mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa morogoro Haule katika uzinduzi wa tovuti na kufunga mafunzo ya uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3) kwa maafisa Habari na Tehama wa halmashauri zote katika mikoa 5.
Hata hivyo amesisitiza kuwa tovuti zilizofunguliwa ni vyema zikafanyiwa kazi kwa kuwekwa habari sahihi na kwa wakati kama ilivyokuwa lengo lake na si kuzitelekeza kwa kutoweka habari za mara kwa mara zinazohusu Halmashauri.
Mafunzo ya uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3) yameanza tarehe 20 mwezi March na kumalizika 27 marchi mwaka huu huku yakihusisha maafisa habari na tehama wa mikoa ya Arusha, Morogoro Simiyu Kilimanjaro na Tanga
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.