Watendaji wa vijiji waratiu elimu kata na wenyeviti wa kamati za shule wilayani malinyi wapatiwa mafunzo juu ya uhamsishaji jamii kuhusu elimu.
Mafunzo hayo yametolewa na shirika lisilokuwa la serikali TUSOME PAMOJA huku wakitakiwa kuwapata watu wawili kwa kila shule ili kuweza kufanikisha suala hilo.
Wakati akizungumza na viongozi hao mmoja wa wawezeshaji ambaye pia ni afisa taaluma elimu msingi FILOTEUS NOMBO amesma kuwa lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kujenga mshikamano kati ya shule na jamii kwenye mchakato wa mpango wa mpango jumuishi wa uhamasishaji wa elimu yaani MJUUE.
Aidha ameongeza kuwa katika mchakato huo wa kuwapata watu hao ni lazima wazingatie uwazi na vigezo vilivyoweka ikiwemo jinsia, elimu, kukubali kufanya kazi kwa kujitolea na watoke katika kamati ya shule pamoja na jamii tofauti.
Hata hivyo wamesisitizwa kuitisha mkutano na kutoa maelekezo kwa wanakijiji na ndani ya siku saba uchaguzi huo uwe umekamilika .
Kwa niaba ya mmoja wa wahudumiaji wa mafunzo hayo mtendaji wa kijiji cha kiswago BEATRICE BUYA ameshukuru mafunzo hayo na kuahidi watayafanyia kazi ndani ya muda huo uliotolewa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo watu kuwa na ugumu mara baada ya kusikia kazi zakujitolea.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.