Wakazi wilayani malinyi wametakiwa kujitoa kikamilifu kuchangia katika masuala ya elimu, afya, miundombinu na ushirika.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Malinyi ndugu Majura Kasika wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa malinyi uliofanyika maeneo ya mjini madukani.
Wakati akizungumza na wakazi hao bwana Majula amesma kuwa katika suala la elimu ufaulu umeongezeka kwa kidato cha nne kutoka asilimia 33 kwa mwaka 2016 mpaka 53 kwa mwaka 2017 hivyo ni vyema kuboresha makambi kwa ajili ya kukaa shuleni.
Aidha katika afya ameeleza kuwa zaid ya billion 1.5 kutoka kwa wahisani I foundation wanatarajia kujenga hospital ya wilaya hukuku million 400 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ngoheranga na 3.9 milion kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa majengo ya zahanati malinyi.
Hata hivyo amewataka vikundi vya vijna na kina mama kujitokeza katika fursa mbalimbali zinazojitokeza huku fedha zitakazokuja zitumiwe ipasavyo kwani serikali ya awamu ya tano siyo ya mchezo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.