Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Majura Kasika amewapongeza wakazi wilayani humo kulima kwa wingi zao la mahindi.
Ameyazungumza hayo kwenye kikao cha hadhara na wananchi kilichofanyika malinyi mjini huku akisema kuwa amefurahishwa sana kwani miaka ya nyuma zao hili lilikuwa halipewi kipaumbele tofauti na mwaka huu.
Aidha ameongeza kuwa kama wilaya matarajio yalikuwa ni kulima hekari 12453 na badala yake hekari zilizolimwa ni zaidi ya 19219 hivyo wamevuka lengo kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo amewataka wakazi hao pia kuhamasika kulima zao la mihogo na pamba kwa kuunda vikundi mbalimbali vya ushirika kwani mazao hayo yameonekana kuwa na soko kubwa nchini China.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.