watumishi wa umma wilayani Malinyi wameaswa kufanya kazi kwa bidii na weredi.
Hayo yameelezwa hii leo na naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa mh Suleiman jafo wakati akizungumza na watumishi wa idara mbalimbali mara baada ya kumaliza kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji makugila, ujenzi wa bweni shule ya sekondari kipingo pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu sekondari ya igawa.
Mh Jafo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali ya utekelezaji hivyo ni vyema kubadilika katika utendaji kazi kwani wengi ni wasomi na serikali imewaamini juu ya hili.
Hata hivyo ameongeza kuwa kila mtumishi ni lazime ajue thamani ya kazi yake ikiwemo kuiheshimu, kufanya kazi kwa umakini na kwa upendo hata kwa watu walio chini yake.
ziara ya naibu waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi wilayani malinyi ni ya siku moja huku lengo likiwa ni kukagua miradi mbalimbali na kuzungumza na watumishi pamoja na viongozi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.