Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bwana Kebwe Steven Kebwe amefanya ziara ya siku mbili wilayani Malinyi ,akiwa katika ziara hiyo tarehe 7/9/2018 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo, vilevile kusikiliza kero na kuongea na wananchi.
Miradi aliyotembelea ni pamoja ujenzi wa barabaraya Kijiji cha Igawa ambayo inajengwa na Tarura wakala wa barabara mjini na vijijini, pia mkuu huyo amekagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ngoheranga unaoendelea na kusikiliza kero za wananchi na kuwaagiza wanakijiji hao kushiriki kikamilifu katika kuongeza majengo ya zahanati hiyo ili waweze kupata huduma za matibabu karibu ,na pia amemwagiza mkuu wa wilaya namkurugenzi wa Halmashauri kutatua mgogoro wa eneo la kanisa ambalo linasadikiwa kuvamiwa na wananchi wa kijiji hicho. Baadaye mkuu wa mkoa amekagua ujenzi wa madarasa matatu ya shule ya Sekondari katika kata ya Kilosampepo na mwisho aliongea na wananchi na kusikiliza kero zao , ambazo ni pamoja na kero ya maji katika kijiji cha Ihowanja. Mkuu huyo pia alihimiza wanawake na vijana kujiunga katika vikundi ili kupata mikopo kutoka Halmashauri ambayo hutolewa katika vikundi na si kwa mtu mmoja mmoja.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.