Baraza la Waheshimiww Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi lapitisha Radimu ya Mpango na Bajeti ya Shilingi Bilioni 30.8 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.
Mkutano huo wa Baraza umefanyika tarehe 10 Februari 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ukiongozws na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Moses Chogo. Kikao hiko pia kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba.
Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kimepitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya kukusanya na kutumia jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 30,808,542,854.00 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2026/2027.
Katika Mchanganuo wa Bajeti hiyo Shilingi Bilioni 1,554,653,000.00 ni matumizi mengineyo kwa fedha za ruzuku ya Serikali Kuu, 17,934,267,800,00 fedha ya ruzuku ya Mishahara kutoka Serikali Kuu, 2,433,436,000.00 kwa Ajili ya Shughuli za Maendeleo kutoka Serikali Kuu na 3,739,286,000.00 kwa Ajili ya Shughuli za Maendeleo kutoka Fedha za Wahisani wa Nje na 5,146,900,054.00 ni fedha ya makusanyo ya Ndani kutoka vyanzo Huru na Lindwa
Aidha katika mwaka wa fedha 2026/2027 Halmashauri imepanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali baadhi ni kama ifuatavyo:-
Kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuimarisha makusanyo ya vyanzo vilivyopo.
Kuweka Mazingira wezeshi ya Uwekezaji.
Kuimarisha upatikanaji wa Huduma za Jamii kama Stendi, Soko, Shule,Madarasa,Minada, Ununuzi wa Madawa nk.
Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Kimkakati (Chikichi, Embe, Kokoa, Korosho) Pia kuongeza Uzalishaji wa Zao la Mpunga ambalo linachangia asilimia 72% ya fedha za makusanyo ya ndani.
Kutoa Mikopo kwa Makundi Maalumu ya Wanawake, Vijana na wenye mahitaji maalumu.
Kuanzisha Radio ya Jamii ndani ya Wilaya ya Malinyi.
Kuwezesha zoezi la ulipaji fidia, upimaji na upangaji wa viwanja eneo la Nyangali awamu ya pili.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.