• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Malinyi District Council
Malinyi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Mipango
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Machine Investment
    • Skimu ya Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili Madiwani
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Kata
      • Biro
      • Igawa
      • Itete
      • Kilosa Mpepo
      • Mtimbira
      • Malinyi
      • Njiwa
      • Ngoheranga
      • Sofi
      • Usangule
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Matamko ya mbalimbali
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video

LENGO LA SERIKALI NI KUHAKIKISHA KUWA UCHUMI UNAENDELEA KUKUA

Posted on: December 10th, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa Wilaya ya Malinyi inategemea sana uchumi wa biashara yaani kilimo biashara, mifugo biashara,uvuvi biashara na ushirika biashaara, hivyo Serikali itahakikisha kuwa kila uchumi unaofanyika Malinyi unakuwa ni uchumi wa kibiashara lengo likiwa ni kuhakikisha uchumi unaendela kukua , mzunguko wa fedha unaongezeka ili Halmashauri ipate mapato, Serikali ipate kodi na Wananchi wapate kipato cha kuendeleza maisha.

Mhe. Waryuba ameyasema hayo Disemba 10, 2024 wakati akifunga kikako cha Baraza la Biashara la Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri

Sambamba na hilo Mhe. Waryuba amewasihi Wadau wa Biashara kutumia Taasisi za fedha kwaajili ya kupata mikopo ambapo maetoa rai kwa Taasisi hizo kuweka mazingira wezeshi ili Wananchi waweze kupata mikopo hiyo kwa urahisi.

“Niwaombe sana sisi ambao tumebeba dhamana ya masuala mbalimbali kwa niaba ya Umma tuhakikishe kuwa Sekta binafsi wanakua ni wadau wetu na ni marafiki zetu, tutengeneze mustakabali huo kwasababu Sekta binafsi wakikaa vizuri na Serikali inakaa vizuri ili mahusiano ya biashara na kiuchumi yaendelee vizuri ndani ya Wilaya ya Malinyi” amesema Mhe. Waryuba

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Biashara Ndugu Msabaha Alawi amesema kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri imeandaa program maalum itakayowashirikisha Wadau wa Biashara kuwajibika kulipa tozo stahiki kwa maendeleo ya Serikali ‘MALIZA MWAKA KIJANJA KWA KULIPA TOZO STAHIKI KWA MAENDELEO YA SERKALI’

Akifafanua kuhusu program hiyo Ndugu Alawi amesema kuwa kuanzia tarehe 11 , Disemba 2024 timu ya Wataalamu itapita maeneo yote ya kibiashara kwa lengo la kutoa elimu ya mifumo ya ulipaji wa tozo stahiki yaani ushuru, ada za leseni za biashara, usajili wa biashara, utoaji wa namba za malipo na utoaji wa leseni hapo kwa hapo, program hiyo inatarajiwa kumalizika tarehe 3/1/2025.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao cha Baraza la Biashara Wadau wa Biashara Wilayani Malinyi wamesema kuwa uchumi wa Malinyi unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja ubovu wa miundombinu ya barabara, na uchache wa vyanzo vya uchumi ambavyo ni kilimo na ufugaji kitu ambacho kinafanya biashara kuwa za msimu na inasababisha uchumi wa Malinyi kutokua imara, kufuatia hali hiyo Wadau hao wameishauri Ofisi ya Mkurugenzi kupitia Divisheni ya Biashara kubuni vyanzo vipya vya kukuza uchumi.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia yote

Habari za hivi punde

  • SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 18 KWAAJILI YA UJENZI WA MADARAJA MAWILI WILAYANI MALINYI

    April 24, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MALINYI YAPONGEZWA KWA UKUSANYAJI WA MAPATO

    April 24, 2025
  • KESI ZOTE ZA MIGOGORO YA ARDHI SASA KUSAJILIWA NA KUSIKILIZWA MALINYI

    March 24, 2025
  • "ITISHENI MIKUTANO YA VIJIJI"

    March 20, 2025
  • Angalia yote

Video

DAS MALINYI AKIKABIDHI PIKIPIKI KWA WARATIBU ELIMU KATA
Video zaidi

Tovuti za haraka

  • Matangazo
  • Habari za Hivi punde

Tovuti Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Tovuti ya Ajira
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2022
  • Matokeo ya Kidato cha Nne
  • SALARY SLIP PORTAL
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

    Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro

    Telephone: 0643111999

    Mobile:

    Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.