Meneja wa NMB Kanda ya Kati Ndugu Janeth Shango amekabidhi msaada wa Viti na Meza 100 pamoja na madawati 100 kwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Kilosa Mpepo tarehe 13 Februari 2026. Msaada huo umehusisha Viti na Meza 100 kwa Shule ya Sekondari Kilosa Mpepo, Madawati 50 kwa Shule ya Msingi Madibira na Madawati 50 kwa Shule ya Msingi Salamiti. Msaada wote ukiwa na thamani ya Shilingi Milioni 21.6.
Akipokea Madawati hayo Mheshimiwa DC Waryuba alieambatana na Kaimu DED Ndugu Christins Chacha na Diwani wa Kata ya Kilosa Mpepo Mheshimiwa Boniventure Kiwanga, ameishukuru sana Benki ya NMB kwa msaada kwa Malinyi na amewakaribisa pia Watu binafsi na Wawekezaji kutoa Misaada katika Sekta ya Elimu na amesema Serikali itaendelea kuiunga mkono NMB kwa juhudi wanazofanya.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati Ndugu Janeth Shango amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya kurudisha faida wanayoipata kwa jamii, wao NMB wakiwa wadau na inatoka kwenye Mfuko wa kusaidia jamii. Ndugu Shango amesema NMB inafahamika kimataifa kama kinara wa wa uwajibikaji kwa Jamii nchini Tanzania. Ni Benki iliyo salama zaidi nchini Tanzania. Benki hiyo ina Matawi 241, ATM-700 na ina Wateja zaidi ya Milioni 8.
Kwa upande wa Meneja wa NMB Tawi la Malinyi Ndugu Anderson Lyatuu ameongelea kuhusu fursa kwa Wazazi na Wanafunzi kuwa NMB wana Chipukizi Akaunti ambayo Mtoto mwenye miaka 13-17 anafungua kwa Shilingi 5000/=
Akitoa shukrani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Diwani wa Kata ya Kilosa Mpepo Mheshimiwa Boniventure Kiwanga ametoa shukrani kwa NMB kwa kuwapatia Viti na Meza 100. Amewashukuru Wanafunzi wa Kilosa Mpepo licha ya changamoto wanafanya vizuri, Shule imetoa Divisheni II tano (5). Ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan, Serikali yake na Chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kuwashika mkono.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.