Mwenge wa uhuru 2023 umeridhia miradi yote iliyotembelewa katika halmashauri ya wilaya ya malinyi mkoani morogoro kuendelea na hatua mbalimbali za umaliziaji kwa miradi iliyowekewa jiwe la msingi huku kwa miradi iliyozinduliwa na kuonwa ikibarikiwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa miradi, Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu 2023 Bwana Abdalah Shaib Kaimu ametoa pongezi kwa mkuu wa wilaya Mh. Sebastian Waryuba kwa kushirikiana vyema na uongozi wa halmashauri hali iliyochangia kufanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Aidha Bwana Kaimu amesifu utuzwaji wa nyaraka za miradi inayoendana na uhalisia wa mradi husika akisema hali hii imemfanya kutokuwa na mashaka yeyote kuhusu utekelezwaji wa mradi husika na hivyo akapongeza juhudi na umakini huo na kumtaka mkuu wa wilaya mh. Waryuba kuendelea kulisimamia hilo ili kila fedha inayotolewa na serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inatumika vyema kwa maslahi mapana ya wananchi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Mh. Waryuba Amemshukuru kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Bwana Shaibu Kaimu na jopo aliloongozana nalo kwa kuridhia miradi yote iliyofikiwa na mwenge na kuahidi kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ambae pia ni Diwani wa kata ya ngoheranga Mh. Pius Mwerase nae amemshukuru kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa na jopo lake kwa kuiridhia miradi yote ya maendeleo iliyotembelewa na mwenge huku akitoa pongezi kwa mkuu wa wilaya Mh Waryuba akisema uzoefu wake katika uongozi ndio chachu ya mafanikio.
Miongoni mwa miradi iliyopitiwa na mbio za mwenge ni pamoja na mradi wa kikundi cha vijana wasakatonge tanga, kizimba cha kuhifadhi taka Misegese, Mradi wa maji Ngoheranga, Klabu ya wapinga rushwa shule ya msingi njiwa, Uzinduzi wa madarasa mawili na ofisi moja shule ya msingi Njiwa, Mradi wa ujenzi wa zahanaji ya kipenyo, Mradi wa matengenezo ya barabara ya benki, miradi hii yote imeridhiwa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2023 wilayani malinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.