1. Kitengo cha Habari, na Mawasiliano kina jukumu la kuhakikisha
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri inadumisha
mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje.
2. Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli
za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,
vitabu, vipeperushi, radio, TV na tovuti.
3. Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia,
kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
Kusimika Mfumo wa Kompyuta wa Kuhifadhi taarifa na
Kumbukumbu za Watumishi na Mishahara (Intergrated
Human Capital Management System); pamoja na utekelezaji wa
Sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi
wa umma
4. Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kupokea na kushughulikia
malalamiko ya wadau yanayohusu Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.