Serikali imepanga kuanza ujenzi wa minara mitano ya Mawasiliano ya simu katika kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro ili kupanua wigo wa upatikanaji wa hudumaza Mawasiliano wilayani humo.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa habari,Mawasiliano na teknolojia ya habari Mh.Nkundo Methew wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo yenye lengo la kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za Mawasiliano ya simu katika maeneo yao.
Akiwa wilayani humo Mh.Methew ametembelea na kuzungumza na Wananchi wa vijiji vya Kilosampepo, Malinyi na Sofi Majiji ambapo amewataka Wananchi wa vijiji hivyo kuilinda na Kuitunza miundo mbinu ya Mawasiliano ya simu iliyopo na itakayojengwa ili waweze kuwa na Uhakika wa kupata huduma za Mawasiliano wakati wote.
Aidha Mh.Methew amewataka Wananchi kutumia huduma ya mitandao ya simu (data)kwa Ajili ya Shughuli za maendeleo na kutojihusisha na makosa ya uhalifu wa mtandao ambayo huweza kusababisha muhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mh.Mathayo Masele amesema hali ya jiografia ya Wilaya ya Malinyi pamoja na sababu zingine za kiufundi ndio chanzo cha upatikanaji duni wa huduma za Mawasiliano katika maeneo mengi wilayani humo.
Minara hiyo ya Mawasiliano ya simu inatarajiwa kujengwa katika kata za Igawa ,Kilosampepo,Itete, Njiwa na Usangule na hivyo kupunguza adha ya Wananchi wa maeneo hayo kuweza kupata huduma ya Mawasiliano wilayani humo.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.