BIASHARA
SHERIA NA TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA LESENI ZA BIASHARA HALMASHAURI YA WILAYA YA MALINYI
S / n
|
SHERIA / KANUNI |
UTARATIBU WA KUFUATWA
|
MUHUSIKA |
MWASILIANO |
1
|
Sheria ya leseni za biashara Na 25 ya 1972
|
Kujaza fomu ya maombi (Fomu Na TFN211) na kuambatanisha nyaraka zifuatazo
- Kwa jina la biashara aweke nakala ya hati ya kuandikisha jina la biashara au kampuni kutoka BRELA - Hati ya uthibitisho wa uraia (Anaweza kuweka cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo cha Mahakama) - Uthibitisho wa kuwa na mahali pa kufanyia biashara( Hati ya nyumba au mkataba wa pango au stakabadhi ya malipo ya kodi ya majengo) - Hati ya kusajiliwa kama Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) - Kwa waombaji ambao sio raia wa Tanzania wawe na hati ya kuishi nchini ya daraja ‘A’ na kwa wawakilishi wa mfanyabishara au kampuni iliyoko nje ya nchi wawe na hati ya Kiwakili ( Power of Attorney) - Kwa biashara za kitaalamu awe na cheti cha utalaamu - Kwa biashara zinazodhibitiwa na Mamlaka za udhibiti awe na hati kutoka Mamlaka husika. Kwa waombaji wanao huisha leseni zao watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita. |
Oscar A. Ramadhani Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0686 467 978 0655347402 |
2
|
Sheria ya leseni za vileo Na 28 ya 1968 na marekebishao yake ya 2012 |
Muombaji atajaza fomu ya maombi
- Atatakiwa kuambataisha Hati ya Mlipa kodi-TIN kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) - Kwa waombaji wapya fomu ipitishwe kwa; a) Serikali ya kijiji b) Kwa Afisa Afya wa kata e) Afisa Biashara - Kwa waombaji wanaohuisha leseni watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita |
Oscar A. Ramadhani Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0686 467 978 0655347402 |
3
|
Hotel levy Act ya 1973 |
Kodi hii hulipwa mara moja kabla ya tarehe 7 ya kila mwezi. Mlipaji anatakiwa kuja na kitabu cha wageni, Afisa Biashara husika hukokotoa kiasi cha kodi kutoka katika kitabu cha wageni. Kiasi cha kodi ni asilimia kumi (10%) ya mapato ya mwezi
|
Oscar A. Ramadhani Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0686 467 978 0655347402 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
5
|
Kodi ya huduma ya Halmashauri; sheria ya Fedha ya Serikali za mitaa sura ya 290 kifungu Na. 6 (01) na 16 (1) |
Kujaza fomu Na. ….. na kuiwasilisha kwa Afisa husika kwaajili ya ukokotoaji wa kiasi cha kodi inayopaswa kulipwa. Tozo ni asilimia 0.3% ya mapato ya kipindi husika.
|
Oscar A. Ramadhani Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0686 467 978 0655347402 |
6
|
Sheria ya afya ya jamii ya 2009 sehemu ya Sehemu ya 27. |
Majengo ya biashara yanapaswa kukaguliwa, Afisa Afya ana uwezo kwa mujibu wa sheria Kufanya Ukaguzi wa kiafya kwenye jengo la biashara, na kujiridhisha na hali ya kiafya ya jengo.
Utaratibu: Waombaji wa leseni za Hoteli za kawaida, Vilabu vya pombe. Watengenezaji na wauzaji wa vyakula na Vinywaji. Majengo wanamo fanyia shughuli hizo yanapaswa kukaguliwa na Afisa Afya: Mwombaji aende kwenye ofisi ya kata husika na aonane na Afisa Afya wa Kata kwaajili ya ukaguzi, kisha kuandaa taarifa ya ukaguzi na kuiwasilisha kwa Afisa Afya Mkuu wa Wilaya, pamoja na maombi ya leseni. |
Afisa afya/Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0753419799/0715368376 |
7
|
Sheria ya afya ya jamii ya 2009 sehemu ya 150 (6) |
Mhudumu / mtumishi yeyote katika nyumba za kulala wageni, hotel au sehemu yoyote inayo tolewa huduma ya vinywaji au vyakula. Anapaswa kupima afya kwa mujibu wa sheria hii.
Utaratibu: Huduma ya kupima afya kwa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi inatolewa katika vituo vya tiba vifuatavyo:- a. Hosipitali ya Lugala |
Afisa afya/Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
0753419799/0715368376 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.