Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mhe, Sebastiana Waryuba amefanya ziara katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha maeneo ya Ulanga - Mahenge.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliambatana na Katibu Tawala (W) Bi Saida Mhanga, Kaimu Mkurugenzi Ndugu John John, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo ni Nyangali, Kitongoji cha Jeshini karibu na madumba, daraja la mchangani, lugala, na kjjiji cha kiwale,
Kufuatia hali hiyo ya mafuriko Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku Wananchi kulima karibu na mito (mita stini kutoka kwenye mto) ili kuilinda kingo za mito zisilete madhara wakati wa masika.
Sambamba na hilio DC Waryuba pia ametoa tahadhari kwa Wakazi wa Malinyi kukaa mbali na maji hayo kwakua ni mengi na yanapita kwa kasi kubwa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Ndugu John John amesema mpaka kufikia jioni ya leo Ofisi yake itatoa maelekezo kuhusu mazingira ya Wanafunzi kwenda shule kwa siku ya kesho Januari 29, 2024 kutokana na baadhi ya shule miundombinu yake kutopitika kirahisi mara baada ya kutokea mafuriko.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.