Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Watendaji wa Kata, Vijiji wapite mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba kuhamasisha wazazi wawapeleke Wanafunzi Shuleni.
DC Waryuba alitoa agizo hilo Januari 8, 2024 alipofanya ziara katika Shule mpya ya Sekondari Kiswago na Shule ya msingi Makugira , agizo hili lilitekelezwa kuanzia Januari 10-15, 2024.
Akiwa katika Shule mpya ya Sekondari Kiswago DC Waryuba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa shule hiyo kupitia mradi wa SEQUIP.
DC Waryuba pia amewashukuru Viongozi wa Kata ya Sofi wakiongozwa na Mhe. Diwani Lucasi Mgonahenga pamoja na Wananchi wa Kata hiyo kwa kukubali kutoa eneo lenye ukubwa wa ekari 33.5 ambalo limetumika kwa ujenzi wa shule hiyo.
Shule mpya ya Sekondari Kiswago imekamilika kwa 90% na imepokea Wanafunzi wapya wa Kidato cha kwanza kwa 50%
Uwepo wa Shule hiyo umesaidia kupunguza umbali wa km 15 ambao Wanafunzi waliokua wakitoka kijiji cha Kiswago na Salamiti waliitembea kwenda shule ya Sekondari Sofi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.