Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amezungumza na Wafanyabiashara Wilayani Malinyi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Wakizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Wafanyabiashara hao wamezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu kuhusu leseni za biashara, tozo za ushuru wa mazao,uhitaji wa mnada katika kijiji cha Misegese, bei ya sukari, ubovu wa miundombinu ya barabara, kuzagaa kwa taka, gharama kubwa za ujazaji wa fomu ya PF3, pamoja na kero ya mawasiliano.
Akijibu kero hizo za Wafanyabiashara, Mhe Sebastian Waryuba ameilekeza Halmashauri kupitia vitengo na Idara zinazohusika kushughulikia kero zilizotolewa na Wafanyabiashara hao kwa haraka na zile kero zinazohitaji kujadiliwa katika vikao vya kisheria zijadiliwe na majibu yatolewe mapema ili kuruhusu shughuli za biasha kuendealea
Sambamba na hilo , Mkuu wa Wilaya ametolea ufafanuzi changamoto ya sukari na kuongeza kuwa changamoto hii ni ya mpito na ina maelekezo maalumu ya Serikali, hivyo amewataka Wafanyabiashara hao kufuata bei elekezi ya Serikali ya shilingi 3000 kwa kilo moja na kwamba kwenda kinyume na bei elekezi ya Serikali ni kutenda kosa la jinai.
Kuhusu uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na athari za mvua zinazoendelea kunyesha DC Waryuba amesema Serikali inapambana kutafuta namna bora ya kufanya mrekebisho na matengezo ya miundombinu hiyo lakini pia ameawataka Watendaji wote wa Kata na Vijiji kuelimisha Wananchi kuacha kufanya shughuli za kiuchumi na makazi mita 60 kutoka kwenye kingo za mito.
Hata hivyo Mhe . Sebastian Waryuba ametumia mkutano huo kutoa msimamo wa Serikali kuhusu mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo ameweka bayana kuwa kutekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani ni kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi, hivyo mfumo huo utaendelea kutumika kama ulivyotumika mwaka jana 2023 lakini Serikali bado inapokea ushauri ili kuuboresha mfumo huo ili uweze kuleta manufaa zaidi kwa Wakulima.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.