Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba wakati akiwasilisha neno la Serikali katika mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili (Oktoba Disemba) uliofanyika Februari 9, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa msingi wa Wilaya ya Malinyi ni kuhakikisha fedha za Serikali zinzoletwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali zinakamilisha miradi hiyo kama ilivyokusudiwa pasipo kuongeza fedha kutoka katika vyanzo vingine.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ndugu Pius Mwelase amesema kuwa miongoni mwa mikakati ya Halmashauri ni kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu 2024/2025 inakamilisha maboma yote yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi.
Sambamba na hilo, ndugu Mwelase amempongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Rose Robert Manumba kwa utendaji wake wa kazi ndani ya muda mfupi tangu aanze kazi rasmi Malinyi na kupekekea Halmashauri ya Wilaya ya Makinyi kupata hati safi.
Masuala mengine yaliyojadiliwa katika Mkutano huo wa Baraza la Madiwani ni pamoja na mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi na tatizo la mgao wa umeme ambao umewashangaza Wahe. Madiwani kwani mgao huo ulianza tangu mwezi wa nane mwaka 2023 kutokana na uhaba wa maji lakini mgao huo bado unaendelea mpaka hivi sasa anbapo mvua zinanyesha kwa wingi na kusababisha mafuriko.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.