Kamati ya Fedha Uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi na baadhi ya wataalam wa Halmashauri wametembelea miradi mbalimbai ya maendeleo inayiotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Raina Paul Mbelembo(Diwani wa kata ya Njiwa)imetembelea mradi wa maji unaotekelezwa katika kata ya Ngoheranga ambao utekelezaji wake upo katika asilimia zaidi ya 90.
Mbali na mradi huo pia wametembelea kikundi cha vijana cha Wasaka Tonge kilichopo katika kata ya Ngoheranga ambacho kilipatiwa fedha za mkpo wa vijana kutoka Halmashauri kiasi cha shilingi milioni 17.2.
Mbali na miradi hiyo pia wamejionea eneo ambalo linatarajia kujengwa kizimba cha ukusanyaji takataka kinachojengwa katika Kata ya Malinyi kwa fedha za mapato ya ndani.
Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mheshimwa Raina Mbelembo amesema kamati imeridhishwa na namna ambavyo wakandarasi wanatekeleza miradi hiyo na kupongeza serikali kutoa fedha za kukamilisha miradi.
“Shilingi milioni 900 zinazojenga mradi wa maji Ngoheranga ni fedha ambazo Mheshimiwa Rais amezitoa kwa ajili ya wananchi wa Malinyi kwa kweli lazima kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwajali wana Malinyi”alisema.
Diwani wa kata ya Malinyi mjini mheshimiwa Said Tira akiwa katika mradi wa vijana ambao wamnunua pikipiki mara baada kupata mkpo wa halmashauri aliwasihi kurejesha mkopo huo kwa wakati kulingana na mkataba wao ili vijana wengine waweze kukopa.
Patrick Mayila ni kaimu mkuu wa Divisheni ya rasilimali watu na Utumishi amewaasa vijana wa kikundi cha Wasaka tonge kubuni pia biashara nyingine kama kilimo ili waweze kujikwamua na umaskini.
“Ni vema wakati mnaendelea na marejesho ya mkopo huu muwe mnafikiria na biashara nyingine ambayo itawasaidia zaidi kuendeleza Maisha yenu lakini kikubwa ni uaminifu na kurejesha mkpo huu kwa wakati”alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi hicho amesema wamejipanga kuanza marejeshi ya mkpo wao kama mkataba wao uavyelekeza ambapo marejesho ya kwanza wanatarajia kufanya mwezi Mei mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.