Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Diwani Lucas Mgomahenga imefanya ziara ya kutembelea mradi wa Shule ya sekondari Ndewele pamoja na ujenzi wa nyumba ya Watumishi (2 in 1) unaoendelea katika shule hiyo.
Kaimu Afisa Mipango wa Wilaya Ndugu Richard Sanga amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza mwaka wa fedha 2021/2022 uligharimu kiasi cha shilingi milioni 470 na kukamilisha baadhi ya majengo na kuongeza kuwa Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imetenga kiashi cha shiling milioni 200 kwaajili ya umaliziaji wa majengo yaliyobakia.
Kutokana na umbali mrefu wanaotembea Wanafunzi wa Shule hiyo Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imeshauri Ofisi ya Mkurugenzi kuandaa utaratibu wa kujenga mabweni katika shule hiyo ili kuwanusuru Wanafunzi hasa Wanafunzi wa kike na kupunguza utoro wa kudumu na utoro wa rejareja katika shule hiyo.
Akizungumzia ujenzi wa nyumba ya Watumishi (2 in 1) unaoendelea katika shule hiyo, Mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari Bi Pendo Masalu amesema mwishoni mwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilipokea fedha shilingi milioni 95 kwaajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya Watumishi ambayo kwa sasa ujenzi bado unaendelea na imekamilika kwa asilimia 68.
Hata hivyo, Imeelezwa kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Wanafunzi kutembea umbali mrefu kutoka kwenye makazi yao, Jamii ya Wafugaji na Wakulima kutokuona umuhimu wa elimu kwa Watoto wao, na uhaba wa maji.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.