• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Malinyi District Council
Malinyi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Mipango
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Machine Investment
    • Skimu ya Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili Madiwani
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Kata
      • Biro
      • Igawa
      • Itete
      • Kilosa Mpepo
      • Mtimbira
      • Malinyi
      • Njiwa
      • Ngoheranga
      • Sofi
      • Usangule
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Matamko ya mbalimbali
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video

Kitengo cha macho hospitali ya wilaya ya malinyi chazinduliwa na kufanya upasuaji wa kwanza

Posted on: March 20th, 2023

Hospitali ya wilaya ya Malinyi imezindua huduma ya kitengo cha macho ambapo sasa kimeanza kutoa huduma rasmi Machi 20 ,2023 na kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba.

Kitengo hicho ambacho kimejengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi million 194 kutoka kwa wafadhili ambao  ni” Eye International Care” mbali ya kujenga kituo hicho pia wametoa ufadhili wa kuwajengea uwezo wataalam wa macho katika hospitali ya wilaya ya Malinyi.

Kulingana na Mganga mkuu wa wilaya ya Malinyi Dkt Aziz Keto kitengo cha macho kwa sasa kimewezeshwa vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia katika utoaji wa huduma za macho za kisasa kuanzia uchunguzi hadi upasuaji.

Upasuaji wa kwanza unatarajiwa kufanyika Machi 21 mwaka huu kupitia wataalamu waliobobea katika sekta  ya macho.

Akizundua huduma katika kituo hicho mkuu wa wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoka zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo sambamba na vifaa tiba

 Amesema kununuliwa kwa vifaa vya kisasa na elimu waliyopatiwa kuhusu utaalamu zaidi wa macho iwe chachu ya kuwahudumia vema wagonjwa wote watakaofanyiwa huduma katika kituo hicho.

Mbali na kuwasisitiza watoa huduma katika kituo hicho kutoa huduma nzuri pia ametoa wito kwa jamii kuanza kula lishe bora ambayo itawasaidia kuondokana na matatizo ya macho.

“Ifikie ndugu zangu sasa tuanze kuhamasisha jamii kula lishe bora ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya macho kwani sasa hivi watu wamekuwa na changamoto ya macho hii inaashiria kuacha kupata lishe bora kwa hito wataalamu wetu wasaidieni jamii kula lishe bora ambayo itawasaidia kutopata matatizo ya macho”alisema.

Awali Katibu Tawala wilaya ya Malinyi Bahati Joram aliwashukuru wafadhili waliojenga jingo hilo shirika la Eye Internationa Care ambao wameshirikiana na halmashauri katika kufikisha malengo ya kufunguliwa kwa huduma ya macho katika hospitali ya Wilaya ya Malinyi.

“Sio hawa wenzetu wa Internationa Eye Care tunakaribisha na wengine waje wawekeze katika huduma za afya wilayani kwetu lengo letu ni ushirikiano mzuri baina ya serikali na mashirika pamoja na watu binafsi”alisema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi  Absalom Gepson Mwasumbwe amesema kulingana na ripoti za kitengo cha macho katika hospitali ya wilayaya Malinyi kitengo cha macho kitapokea wagonjwa kutoka katika zahanati mbalimbali wilayani humo,vituo vya afya na hatimae wale ambao watagundulika na matatizo ya macho watapewa huduma zote katika kitengo hicho bila kufuata tena huduma katika wilaya zingine ama mikoa mingine.

Diwani wa kata ya Malinyi Mheshimiwa Said Tira ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati za huduma za jamii amesema wananchi wa Malinyi hawajutii kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo kwani sasa matunda yameanza kuonekana.

“Nimshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae ametupatia vifaa vya kisasa kabisa katika hospitali hii ambapo vingine vimeshaanza kutumika katika hospitali hii hakika ni jambo la kujivunia sana”alisema.

Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi huo wameishukuru serikali kuwezesha vifaa katika kitengo hicho na kusema sasa wataepukana na adha ya kufuata huduma ya macho nje ya wilaya ya Malinyi.

“Jambo hili la kupongezwa sana kwa maana sasa tutakuwa tumepata unafuu kupata huduma hapa hapa katika hospitali yetu “alisema Bi. Mariam Malambo mkazi wa Kijiji cha misegese.

Ally Samadu mkazi wa mwembeni Malinyi anasema kuanza kufanya kazi kwa hospitali ya wilaya kwa baadhi ya vitengo kumewarahisishia upatikanaji wa huduma za afya hasa wagonjwa waliokuwa wanatoka mbali na wasio na uwezo mkubwa kiuchumi.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2020/2021 December 18, 2020
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2020 January 17, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI January 18, 2021
  • Tangazo la Nafasi za kazi May 26, 2022
  • Angalia yote

Habari za hivi punde

  • Mwenge wa uhuru 2023 umeridhia miradi yote yenye thamani ya shilingi milioni 825.8 Malinyi

    May 08, 2023
  • Kamati ya fedha mipango na uongozi Malinyi yatembelea miradi ya maendeleo

    April 18, 2023
  • Kitengo cha macho hospitali ya wilaya ya malinyi chazinduliwa na kufanya upasuaji wa kwanza

    March 20, 2023
  • Kitengo cha macho hospitali ya wilaya ya malinyi chazinduliwa na kufanya upasuaji wa kwanza

    March 20, 2023
  • Angalia yote

Video

DAS MALINYI AKIKABIDHI PIKIPIKI KWA WARATIBU ELIMU KATA
Video zaidi

Tovuti za haraka

  • Matangazo
  • Habari za Hivi punde

Tovuti Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Tovuti ya Ajira
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2022
  • Matokeo ya Kidato cha Nne
  • SALARY SLIP PORTAL
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

    Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro

    Telephone: 0643111999

    Mobile:

    Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.