Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba April 18, 2024 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Malinyi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Katibu wa CCM Wilaya,Wataalam kutoka Halmashauri(Mratibu wa Mwenge Wilaya,Mhandisi,Afusa Elimu Msingi)
Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa miradi utakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ina thamani ya shilingi milioni 401 ambayo ni mradi wa vijana Tumaini, Mradi wa miche, Jengo la mionzi katika Kituo cha Afya Mtimbira, Shule ya msingi Kiswago ( madarasa mawili, matundu 4 ya vyoo) na Mradi wa maji wa Sofi Misheni.
Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya amebainisha kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 94 ndani ya Wilaya ya Malinyi.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe, Sebastian Waryuba alitembekea kikundi cha Vijana wa Halaiki ambapo Vijana hao zaidi ya mia moja kutoka Shule ya msingi Mtimbira, Shule ya Msingi Madibira na Shule ya Msingi Madibira juu walimuonyesha Mkuu wa Wilaya jinsi walivyojiweka tayari kwa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Malinyi.
Wilaya ya Malinyi inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru April 25, 2024 katika Kata ya Itete Mesheni kutoka Wilaya ya Ulanga, Mwenge utakimbizwa ndani ya Wilaya ya Malinyi kwa umbali wa kilometa 94 ambapo mkesha wa Mwenge wa Uhuru utafanyika katika Kata ya Mtimbira na April 26, 2024 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji Ifakara.
KAULI MBIU: "TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDEKEVU
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.