Mkuu wa Wilaya ya MalinyIi Mhe. Sebastian Waryuba leo April 19, 2024 ameongoza zoezi la kufanya usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti katika Hospitali ya Wilaya ya Malinyi ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani yanayotarajiwa kufanyika April 26, 2024.
Katika zoezi hilo DC Waryuba ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya Bi Saida Mhanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Joseph Ogare, pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo kutoka Halmashauri.
Akizungumza mara baada ya kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti katika Hospitali ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wilaya ya Malinyi imefanya uzinduzi wa upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira, kufanya usafi wa mazingira na kuhimiza Jamii kuendeleza zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kuwa mazingira ndiyo maisha yetu.
Aidha, Mhe. Sebastian Waryuba amefafanua kuwa zoezi hili la usafi wa mazingira na upandaji miti limefanyika ili kuunga mkono kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru unaosema "Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endekevu"
Sambamba na hilo, Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Wakazi wa Malinyi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa kugombea nafasi mbalimbali na kuchagua viongozi imara watakaosaidia kuijenga Wilaya ya Malinyi na Taifa kwaujumla.
KAULI MBIU YA MWENGE WA UHURU:Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endekevu"
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI : Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa letu”.*
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.