Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapatia Wananchi wa Wilaya ya Malinyi gari jipya kwaajili ya matumizi ya kubebea Wagonjwa (Ambulance).
Makadhiano ya gari hilo yamefanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi na kushudiwa na Wahe. Madiwani (Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango) pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa niaba ya Watumishi.
Akikabidhi gari hilo kwa Mkuu wa Wilaya, Mbunge wa Wilaya ya Malinyi Mhe, Antipas Mgungusi amesema hapo awali aliomba magari manne (4) ya kubebea Wagonjwa (ambulance) kwaajili ya kituo cha Afya Ngoheranga, Itete, Mtimbira, na Hospitali ya Wilaya lakini kutokana mambo ya bajeti amepokea gari moja kutoka TAMISEMI na kuongeza kuwa Wizara ya Afya imeahidi kuwapatia Wananchi wa Malinyi gari jingine la kubebea Wagonjwa ndani ya miezi miwili ijayo.
Mhe. Mbunge amesema ana imani na Mkuu wa Wilaya Mhe. Sebastian Waryuba na Mkurugenzi Mtendaji Rehema Basi kuwa gari hilo litatumika kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa na Mhe. Rais ya kusaidia Wananchi wa Wilaya ya Malinyi katika sekta ya Afya.
Aidha, mara baada ya kupokea gari hilo kutoka kwa Mhe. Mbunge wa Wilaya ya Malinyi, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba naye alikabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Said Bwasi na kusisitiza kuwa gari hilo ni kwaajili ya Wagonjwa na matumizi ya Hospitali ya Wilaya hivyo Halmashauri ina wajibu wa kulitunza gari hilo na kuhakikisha kuwa linatumika kwa matumizi sahihi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Said Bwasi amesema Malinyi hakukua na gari la kubebea Wagonjwa (ambulance) na ilikua vigumu sana kwa Wagonjwa kupata huduma hii, lakini adha ya kubeba Wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya kwasasa imekwisha kutokana na ujio wa gari hilo.
"Ninakiri kupokea gari hili jipya kabisa mbele ya Mhe. Mkuu wa Wilaya, Mhe Mbunge, Wahe. Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo ambao mpo hapa kwa niaba ya Watumishi kushuhudia tendo hili kubwa, na ninaahidi kulitunza na kuhakikisha linafanya kazi sahihi kama ilivyokusudiwa" amesema Bi Rehema Bwasi.
Mhe. Mbunge, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji Wamemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kugusa shida za Wananchi wa Malinyi.
ASANTE MAMA
KAZI IENDELEE
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.