leo April 20, 2024 Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Morogoro ukitokea Mkoani Tanga teyari kuanza kukimbizwa kwa siku tisa Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Batlda Burian.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokekelewa Wilayani Malinyi Apri 25, 2024 katika Kata ya Itete Misheni kutoka Wilaya ya Ulanga.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 94 ndani ya Wilaya ya Malinyi na utapitia miradi mitano (5) yenye thamani ya shilingi Milioni 401.
Miradi itakayopitiwa na Mwenge Wilayani Malinyi ni Mradi wa maji uliopo Sofi Misheni, Mradi wa miche, Mradi wa Vijana Tumaini, Jengo la Mionzi lilopo katika Kituo cha Afya Mtimbira, na Shule ya Msingi Kiswago(madarasa mawili na matundu ya vyoo 4)
Mkesha wa Mwenge wa Uhuru utafanyika Mtimbira ambapo April 26, 2024 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
KAULI MBIU YA MWENGE WA UHURU 2024 "TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.