Januari 17, 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kupitia Idara ya Elimu Sekondari imefanya mkutano na Wananchi wa Kata ya Mtimbira ili kuchagua na kukubalian eneo itakapojengwa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Mtimbira Willaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.
Mkutano wa makubaliano hayao ulihudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bi Saida Mhanga ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mallnyi, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bi Pendo Masalu, Viongozi wa Kata ya Mtimbira wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Bi Jane Komba, Madiwani wa Viti maalum Bi Stamili Kiponda, Bi Consolata Chambuya, Katibu Tarafa Ndugu Leopold Ngakoka, Viongozi wa CCM, Mwenyekiti Ndugu Rahimu Mkombachepa, Mkuu wa Shule ya Sekondary Mtimbira Ndugu Ackrey Melchior Lyotela pamoja na Wananchi wa Kata ya Mtimbira.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kipenyo na maeneo jirani ambayo yapo ndani ya Kata ya Mtimbira Mkuu wa Divishheni ya Elimu Sekondari Wilaya ya Malinyi Bi Pendo Masalu amewataka Wananchi hao kuchagua eneo lisilo na mgogoro wa ardhi kwani Serikali haiwezi kujenga eneo lililo na mgogoro na kuongeza kuwa lengo la Shule hiyo mpya ni kupunguza msongamano wa Wanafunzi katika Shule ya Sekondarib Mtimbira pamoja na kuwapunguzia Wanfunzi umbali mrefu wa kutembea kutoka nyunbani kwenda Shuleni.
Katika kikao hicho Wananchi walipewa nafasi ya kutoa maoni yao na walipendekeza shule hiyo mpya ya Sekondari ijengwe katika Kijiji cha Udeko Kipenyo ambapo Serikali ya Kijiji imetoa eneo lenye ukubwa wa ekari 50 kwaajili ya ujenzi wa Shule hiyo.
Mara baada ya kukubaliana eneo litakapojengwa Shule hiyo, Katibu Tawala, Mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari, Viongozi wa Kata wakiongozwa na Wahe, Madiwaani pamoja na Wananchi walielekea katika eneo lilichaguliwa kwaajili ya ujenzi wa Shule hiyo ili kulifanyia ukaguzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.